July 5, 2017


Kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Mwarami Mohammed ndiye kocha mpya wa makipa wa Simba.

Mwarami anachukua nafasi ya Mkenya Iddi Salim ambaye yuko nchini Kenya alikorejea kwa mapumziko.

Kupitia kurasa zao za mitandao, klabu ya Simba imemtangaza Mwarami ambaye amekuwa kocha wa timu za taifa za vijana kuwa kocha mpya wa makipa.


Mwarami ambaye aliwahi kuidakia Simba, atajiunga na kikosi cha Simba mara moja kitakapoanza maandalizi ya msimu mpya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV