July 5, 2017Kiungo wa pembeni mwenye uwezo wa kucheza kama mshambuliaji, Pastory Athanas ameamua kung'oa nanga Simba na kutua kwa matajiri wapya wa Singida United FF.

Athanas ambaye ameichezea Simba msimu mmoja tu akitokea Stand United ya Shinyanga hakuwa na nafasi ya uhakika Simba hadi alivyotua Singida, hii leo akisaini mkataba wa miaka miwili.

Mshambulizi huyo, alikabidhiwa jezi yake rasmi yenye maandishi SportPesa kifuani na Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga.1 COMMENTS:

  1. mbona kuna wadhamini weengi tu hapo kaka? sio sportpesa peke yao, huwaoni hata Halotel, Puma energy, Oryx na NMB??

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV