August 10, 2017


Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Yanga, Aaron Nyanda, amejinadi kupitia Global TV Online katika nafasi anayogombea katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) ya kuwa mjumbe wa Kanda ya Ziwa.

Nyanda amesema dhamira yake katika nafasi hiyo ni kutaka kujumuisha kwa pamoja juhudi za kuinua soka katika eneo hilo la nchi badala ya kila timu au vyama vya eneo hilo kufanya mambo kipekee.


Akizungumzia kuhusu kutofuatwa kwa ratiba za mechi za Ligi Kuu, Nyanda alisema ni lazima TFF iwe na ifuate kalenda au ratiba za mashirikisho ya soka duniani kama vile Fifa, Caf, Cosafa kama ikitokea nchi imealikwa, na kadhalika.



Alisema mchakato huo lazima ushirikishe wataalam wa masuala ya soka kwa pande zote, zikiwemo klabu husika ili kuondoa malalamiko.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic