August 8, 2017Unaweza ukasema, yaleyake. Mario Balotelli hakui maana kila siku, vituko tu.
Safari ameng’ang’aniwa na Polisi baada ya kuendesha gari lake mwendo kasi kupitiliza hadi kufikia mail 125 kwa saa.
Balotelli alikuwa akiendesha gari aina ya  Ferrari, amekamatw ana Polisi nchini Italia.

Mshambuliaji huyo wa Nice ya Ufaransa, alikuwa akikimbia kwa kasi hiyo huku akijua hairuhusiwi kufanya hivyo.

Polisi hao waliokuwa katika eneo la Vicenza walifanikiwa kumkimbiza na kumsimamisha kabla ya baadaye kumkamata.


Moja ya faini aliyopigwa ni kwa kuwa gari lake limesajiliwa mwendo mkubwa kuwa ni maili 105 kwa saa na si zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV