August 11, 2017


Mshambuliaji nyota Juventus, Paulo Dybala sasa anafuata nyayo za gwiji la klabu hiyo, Alessandro Del Piero.

Dyabala ameamua kuachana na jezi namba 21 iliyokuwa maarufu baada ya kutumiwa na Zinedine Zidane na baadaye Paul Pogba.


Sasa anaingia katika namba 10 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Del Piero anayeaminika ndiye kipenzi zaidi cha mashabiki wa klabu hiyo katika karne ya 21.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV