August 11, 2017



Kiungo wa Simba, raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima ameweka wazi kuwa yeye ndiye aliyemuomba kiungo mkongwe wa timu hiyo, Mwinyi Kazimoto amuachie jezi namba nane aliyokuwa akiitumia msimu uliopita.

Niyonzima amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Yanga baada ya mkataba wake kumalizika Julai 21, mwaka huu huku akigomea kusaini timu yake ya zamani kutokana na kushindwana katika dau la usajili.

Kazimoto amekuwa akitumia jezi namba nane tangu msimu uliopita lakini ameamua kubadilisha na kuchukua namba 24 iliyokuwa ikitumiwa na Abdi Banda aliyejiunga na Baroka FC ya Afrika Kusini.

Niyonzima amesema aliamua kumuomba jezi hiyo kwa kuwa tangu aanze kucheza soka hajawahi kuvaa jezi yenye namba tofauti na hiyo jambo ambalo linamuongezea bahati uwanjani.

“Kwangu limekuwa ni tukio zuri kwa sababu kwanza kabisa Kazimoto namkubali kwa kuwa ni mchezaji mzuri na mkubwa ambaye namuheshimu, kilichotokea ni kwamba mimi mwenyewe nimemuomba na ameridhia kunipa jezi namba nane bila ya kinyongo chochote.


“Kiukweli ni kitu cha kumshukuru maana sikutarajia na nimemuahidi kwamba nitamtafutia zawadi kwa sababu amenifanya nijisikie kucheza kwa amani nikiwa ndani ya jezi namba nane maana tangu nianze kucheza mpira ndiyo nimekuwa nikiivaa sijawahi kubadilisha namba,” alisema Niyonzima.

SOURCE: CHAMPIONI 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic