August 11, 2017
RUVU Shooting ya mkoani hapa, imesema kikosi cha Simba kilichocheza na Rayon Sports ya Rwanda, Jumanne wiki hii, hakina uwezo wa kuwafunga katika mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara Agosti 26, mwaka huu.


Katika Tamasha la Simba Day, Simba iliifunga Rayon bao 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema kama kuna mashabiki wanakiona kikosi cha Simba ni kizuri, basi wamepotea kwani wao wanakiona cha kawaida kisichoweza kuwasumbua.


Bwire ametamba kuwa wataishushia kipigo kikali Simba watakapokutana kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu itakayoanza Agosti 26, mwaka huu.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV