August 9, 2017Mgombea wa nafasi ya urais katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Imani Omar Madega, amezindua rasmi kampeni zake leo kwenye Hoteli ya New African, Posta jijini Dar.

Madega katika uzinduzi huo amesema kutokana na kuwa na uzoefu na matatizo ya soka,  hana woga wa kuyatatua akipata ridhaa ya kuwa rais.

    Wanahabari wakiendelea kumsikiliza Madega.

Aidha Madega alisema, ni mzoefu wa masuala ya soka kutokana na kuwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Pwani (Corefa) na atautumia uzoefu huo kufanikisha soka linapiga hatua zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV