August 9, 2017Mchezaji wa zamani wa Yanga, Ally Mayai ambaye anawania nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), amezindua kampeni zake kwenye Ukumbi wa Ramada Posta jijini Dar es Salaam, huku akitaja vipaumbele kadhaa.Mayai amesema endapo akipata nafasi ya kuwa rais wa shrikisho hilo atahakikisha analisimamia soka vizuri kuanzia ngazi ya vijana, wanawake na ngazi ya juu kwa welendi.“Nataka kuona soka linasimamiwa kwa weledi kila mtu afanye kazi kuhakikisha kuwa soka letu linakuwa kuanzia ngazi ya vijana, wanawake na ngazi ya juu.“Pia nitahakikisha kunakuwa na uanzishwaji wa Academi nyingi na zinazosimamiwa vyema,” alisema Mayai. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV