August 1, 2017



Kiungo kinda wa pembeni wa Difaa Al Jadid ya Morocco, Ramadhani Singano Messi ameonyesha kuwa kivutio baada ya mechi yake ya kwanza ya kirafiki akiitumikia klabu hiyo.

Mechi hiyo Difaa Al Jadid ilipoteza kwa mabao 2-1 huku Mtanzania mwingine, Simon Msuva akifunga bao la kufutia machozi.

Lakini wachambuzi kadhaa wa soka wameonyesha kuvutiwa na Singano ambayo alicheza kwa kujiamini na kutoa msaada mkubwa.

Katika uchambuzi wa runinga moja ya michezo, zaidi wameeleza alivyokuwa mwepesi kutoa pasi na kuchukua nafasi na mwisho kujumuisha kwamba, “Watanzania hao wakizoea Ligi ya Morocco, watakuwa hatari zaidi”.


Singano amejiunga na timu hiyo akitokea Azam FC baada ya mkataba wake kumalizika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic