August 28, 2017




Pamoja na mwanamasumbwi, Conor McGregor kupokea kipigo cha TKO katika raundi ya 10 kutoka kwa Floyd Mayweather, takwimu zinambeba na kumfanya kuwa bora hats kuliko Manny Pacquiao.

McGregor anaonekana anafanya vizuri alivyokutana na Mayweather kuliko bondia huyo ambaye hajapigwa mechi hata moja katika 50 za kulipwa, alipokutana na Pacquiao.

Kumbuka McGregor ni mpiganaji wa mchezo wa ngumi na mateke na ilikuwa mara ya kwanza anapigana ngumi za kulipwa bila mateke.

Takwimu zinaonyesha, McGregor alipiga ngumi 111 dhidi ya Mayweather ambaye yeye alimpiga McGregor ngumi 430.


Katika pambano ambalo lilifanyika mwaka 2015, Pacquiao alimpiga Mayweather ngumi 89 wakati Mfilipino huyo aliruhusu ngumi 429 kutoka kwa Mayweather.


Kwa hesabu zinaonyesha kuwa McGregor, alifikisha asilimia 26 ya ngumi kwenye mwili wa Mayweather huku Pacquiao akiwa amefikisha asilimia 19 tu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic