September 24, 2017




Singida United imepata ushindi wake wa tatu baada ya kuitwanga Kagera Sugar kwa bao 1-0.

Singida imeibuka na ushindi huo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, hii ikionyesha kuwa wamekaa vizuri.

Kikosi cha Singida United kilichoanza kwa kupoteza mechi ya kwanza, kimeamka na kuanza kwa kupata ushindi wake wa tatu mfululizo.

Kocha Hans van der Pluijm ambaye alirejea katika benchi lake baada ya kumaliza adhabu yake, amesema anaanza kuona mwanga.

“Mwanga unaonekana na vile tunavyovifanyia kazi vinaanza kuonekana. Bado kuna mambo ya kurekebisha na kuendelea kufanya vema,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic