September 24, 2017


Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema anaamini wataamka na kufanya vema.

Maxime amesema hayo baada ya kupoteza mechi ya tatu ya Ligi Kuu Bara ligi ikiwa mbichi kabisa.

Kagera Sugar wamepoteza mchezo wao wa tatu baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji wao, Singida United.

"Katika mpira kila kitu tunajifunza ndiyo maana tunafanya mazoezi, lakini kweli hatuko vizuri sana na tunatakiwa kujituma na kujitutua.

"Bado nina imani tutasimama na kufanya vizuri. Tunajituma sana lakini bado mambo hayajakaa vizuri."


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic