September 26, 2017


Kesi ya utumiaji wa dawa ya kulevya inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji jana Jumanne iliendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Daktari Mfawidhi wa Gereza la Keko, Inspekta Eliud Mwakawanga alitoa ushahidi wake juu ya mtuhumiwa huyo jinsi alivyokuwa anatumia dawa mbalimbali akiwa ndani ya Gereza hilo.

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha, Dk Mwakawanga amesema kuwa alianza kumfahamu Manji tangu Julai 6, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alienda kumjulia hali kutokana na kufikishwa hapo kabla ya kupelekwa ndani ya gereza hilo.

“Manji nimeanza kumfahamu tangu Julai 6, alipolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo alikuwa amelazwa na afya yake haikuwa nzuri, mara kadhaa wakati yupo gerezani Keko alikuwa anatumia dawa kwa wakati wote ambao alikuwepo hapo.

“Kwa siku alikuwa anatumia vidonge vya dawa kati ya 20 hadi 25 kutokana na hali yake kuwa mbaya, na muda mwingine vidonge vyake viliagizwa kutoka nje ya gereza kwa sababu havikuwepo ndani ya hospitali ya gereza, Kuna baadhi ya vidonge havikuwepo kabisa ila nilionyeshwa cheti chake kuatoka kwa daktari wake wa Marekani.

“Tangu nimempokea halia yake kiafya haikuwa nzuri  na alikuwa anayetumia dawa wakati wote, alikuja na dawa zake za aina sita kutoka Muhimbili ambazo alikuwa akizutumia kulingana na hali yake na mazingira anayojisikiaa lakini tulikuwa tunampatia dawa nyingine mbali na hizo, sisi hatutoi dawa za kulevya ila tunatoa dawa,”alisema.


Mbali na inspekta huyo mashahidi wengine waliotoa ushahidi katika kesi hiyo ni Sekretari wa Manji katika kampuni ya Quality Group, Maria Theresia Makwaiya, na Daktari Bingwa wa Afya ya Akili na Dawa za Kulevya kutoka Hospitali ya Rufaa Temeke, Francis Benedict ambaye hakukubaliana na ripoti ya mkemia mkuu juu ya madawa zilizokutwa kwenye mkojo wa Manji, alipoulizwa na wakili wa utetezi, Hajra Mangula.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic