September 26, 2017



 Kesi ya tuhuma za kutumia madawa ya kulevya inayimkabiri Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Yusuf Manji, inaendelea kuunguruma tena leo.

Kesi hiyo katika suala la kutoa ushahidi upande wa mshitakiwa ulianza jana na itaendelea kwa siku tatu, yaani leo, kesho na keshokutwa.

Manji ameanza kujitetea hiyo jana mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu kesi yake ya dawa za kulevya inayomkabili.

Kesi hiyo ambayo imepangwa kusikilizwa kwa siku tatu mfululizo kwa upande wa ushahidi kuanza kutoa utetezi wao ambao leo imekuwa ni siku ya kwanza  kwa mashahidi watatu akiwemo Manji mwenyewe.

 Licha ya mwenyekiti hiyo wa zamani wa Yanga na diwani wa kata ya Mabagala KUU  kutoa utetezi wake wengine walikuwa Daktari wa Hospital ya Aga Khan, Profesa Mustapha Bapumia na bingwa wa magonjwa wa Toto, DR Khan.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic