BAADA ya kutoka suluhu na Simba, kiungo mshambuliaji wa Azam
FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, amefunguka licha ya usajili wa Simba kutumia
mabilioni ya shilingi lakini timu hiyo imekuwa na uwezo mdogo uwanjani.
Simba
inatajwa kutumia jumla ya Sh bilioni 1.3 katika usajili wake wa msimu huu na
kupelekea kuwa kikosi ghali zaidi kikiwa na mastaa mbalimbali akiwemo Emmanuel
Okwi, John Bocco na Haruna Niyonzima.
Sure Boy ameyasema hayo kufuatia kutoka
sare ya bila kufungana na timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa
juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Azam Complex ulipo Chamazi nje
kidogo la Jiji la Dar. Akizungumza Sure Boy alisema kuwa hakutarajia
wapinzani wao kucheza katika kiwango cha kawaida kama ilivyotokea kwa
kuwa wana timu inayodaiwa kusajiliwa kwa pesa nyingi.
“Mechi haikuwa rahisi na
wala haikuwa ngumu sana ila tunashukuru kwa matokeo ambayo yametokea,
tulijipanga kushinda mchezo wa leo (juzi) lakini haikuwa bahati kwa sababu
ukiangalia sisi ndiyo tulikuwa bora zaidi ya wenzetu na tulistahili kushinda.
“Simba naweza kusema imecheza kwenye kiwango
cha kawaida sana kwa sababu
tumemiliki mpira na kufanya mashambulizi ya maana zaidi yao, ndiyo maana
nasema ya kawaida kwani imekuwa tofauti na thamani yake inayosemwa,” alisema
Sure Boy.
Akapimwe mkojo huyu dogo..stats zinaonesha Simba,walikuabvizuri zaidi..
ReplyDelete