October 31, 2017




Mambo yamezidi kuwa magumu kwa mshambuliaji Donald Ngoma baada ya kushindwa kuanza mazoezi kama ilivyotegemewa.

Ngoma bado ni majeruhi kama ilivyo kwa kiungo Thabani Kamusoko ambaye naye hajaanza mazoezi Yanga.

Maana yake, Ngoma, Kamusoko pamoja na mshambulizi mwingine, Amissi Tambwe hawatacheza mechi ya wikiendi ijayo wakati Yanga itakapoivaa Singida United.

Watatu hao ambao wamekuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza, waliikosa mechi dhidi ya watani wao Simba ambayo iliisha kwa sare ya bao 1-1 huku Yanga ikionyesha soka safi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic