October 30, 2017

CHIRWA



Bosi wa benchi la ufundi la Simba, Mcameroon, Joseph Omog, amemwagia sifa mshambuliaji wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha uwanjani juzi Jumamosi katika mchezo uliozikutanisha timu hizo.

Yanga na Simba zilikutana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu Bara na matokeo yalikuwa ni sare ya kufungana bao 1-1.

Bao la Yanga katika mechi hiyo lilifungwa na Chirwa wakati lile la Simba lilifungwa na Shiza Kichuya.

Omog amesema kuwa, Chirwa ndiye mchezaji wa Yanga aliyeisumbua vilivyo safu yake ya ulinzi kuliko mchezaji yeyote wa timu hiyo.

OMOG

Alisema alikuwa anapata wasiwasi kila alipokuwa akishika mpira na kuanza kuukokota kuelekea langoni kwao lakini anawapongeza mabeki kwa kujitahidi kukabiliana naye.

“Chirwa yupo vizuri na ndiye mchezaji wa Yanga aliyekuwa akinipatia wasiwasi kila alipokuwa akishika mpira.
“Hofu hiyo ilikuja kutokana na kasi yake kubwa lakini pia uwezo wake mkubwa wa kushindana nguvu na mabeki wangu ambao alikuwa akiwashinda kila wakati.

“Hata hivyo yote kwa yote nawapongoza mabeki wangu kwa kazi kubwa waliyoifanya uwanjani,” alisema Omog.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic