October 13, 2017



Kocha George Lwandamina analazimika kuingia katika mipango mingine kabisa baada ya kuumia kwa kiungo wa wake Thaban Kamusoko, raia wa Zimbabwe.

Lwandamina raia wa Zambia analazimika kuanza upya mipango yake kwa kuwa alitarajia Kamusoko angerejea na kuungana na wenzake baada ya kucheza mechi iliyopita akiingia.

Hata hivyo, mambo yamekuwa tofauti baada ya Kamusoko kutakiwa kupumzika kwa wiki mbili.

Yanga kwa sasa ipo vitani ikiwania kurudi kileleni kutokana na kuwa na pointi tisa hadi sasa ikiwa nafasi ya sita huku wapinzani wao Simba wakiongoza kwa kuwa na pointi 11 sawa na Mtibwa, hivyo kuwa na wachezaji majeruhi ambao ni tegemeo katika kikosi cha kwanza ni pigo na kunaigharimu timu.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema Kamusoko atalazimika kukosa michezo miwili iliyo mbele yao dhidi ya Kagera na Stand kutokana na majeraha ambayo yatamuweka nje wiki mbili.

“Kamusoko hayupo katika mpango wa safari ya leo (jana) kutokana na kuumwa kifundo cha mguu ambapo leo ana siku ya nne tangu alipoanza kuumwa, hivyo atalazimika kukaa wiki mbili na kukosa michezo miwili dhidi ya Kagera na Stand.

“Timu itakuwa huko kwa muda wa wiki mbili hadi itakapomaliza mchezo wake dhidi ya Stand, naamini baada ya hapo atakuwa fiti kwa ajili ya kujiunga na wenzie.


“Kwa upande wa Ngoma yeye atakuwemo safarini lakini mechi dhidi ya Kagera hatacheza, atakuwa anaendelea na matibabu na mazoezi mepesi lakini anatarajiwa kucheza katika mechi ijayo dhidi ya Stand,” alisema Ten. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic