October 15, 2017







Kampuni ya StarTimes Tanzania, jana Jumamosi na leo Jumapili, iliendesha zoezi la kusaka washiriki 10 kutoka jijini Dar, watakaoshiriki Shindano la Vipaji vya Sauti ambapo katika usaili huo, zaidi ya washiriki 2500 walijitokeza.


Katika zoezi hilo lililofanyika kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar, watu mbalimbali maarufu walijitokeza akiwemo Abdallah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’.

Afisa Mahusiano wa StarTimes Tanzania, Samweli Gisayi, amesema usaili huo kwa wakazi wa Dar, umekuja baada ya kuwapata washiriki watano kutoka Zanzibar na watano jijini Mwanza.


“Baada ya kuwapata washiriki watano kutoka Zanzibar na watano kutoka Mwanza, tunamalizia Dar ambapo tunachukua washiriki kumi ambao jumla watakuwa 20.


“Hao washiriki 20, watashindana kwenye fainali ambayo itafanyika jijini Dar Oktoba 27, mwaka huu. Tunahitaji washindi kumi pekee ambao wataenda China kufanya kazi mwaka mmoja ya kuingiza sauti za Kiswahili kwenye filamu za Kichina.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic