October 15, 2017


Mazoezi ya Simba ya jana yanaonyesha timu hiyo itacheza kwa kasi kuhakikisha inawadhibiti Mtibwa Sugar.

Lakini kivutio zaidi kinaonekana kitakuwa ni katikati ya uwanja wakati Simba yenye viungo wengi bora itakuwa ikipambana na Mtibwa yenye viungo bora pia.

Mtibwa Sugar wanaonekana ni bora zaidi katika kiungo eneo ambalo Simba wanacheza kwa kiwango cha juu.

Katika mazoezi ya mwisho jana ya Simba kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Omog alionyesha wazi alitaka timu yake icheze mpira “mwingi” kuhakikisha inakaa na mpira muda mwingi.

Kawaida, unapokuwa na mpira kwa sayansi ya soka inaonekana uko salama zaidi hata kama haushambulii.









0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic