October 15, 2017



Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu ndiye mshambuliaji gumzo zaidi kwa sasa katika Ligi Kuu Bara na hii inachangiwa na ile ishu ya Lionel Messi.

Ajibu amekuwa gumzo zaidi baada ya kufikisha mabao matatu akiifungia Yanga katika mechi dhidi ya Kagera Sugar katika ushindi wa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Katiba, Bukoba.



Bao hilo limekuwa la tatu kwa kuwa linaiwezesha Yanga kubeba pointi tisa kupitia mabao matatu ya Ajibu.
Gumzo la Ajibu limezidi kupaa baada ya mchezaji huyo kuvua jezi yake namba 10 na kuwaonyesha mashabiki waliokuwa uwanjani hapo.

Ajibu alifanya hivyo akiiga mfano wa Messi ambaye aliwafunga Madrid bao la tatu dakika za mwisho kabisa msimu uliopita na kuwaonyesha mashabiki waliokuwa Santiago Bernabeu jezi yake namba 10.


Kutokana na kitendo hicho, gumzo limekuwa kubwa kitandaoni huku mashabiki wakijadili wengine wakionyesha kukerwa na wengine wakifurahia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic