October 26, 2017



Wakati Simba wanajifua Uwanja wa Amaan, watani wao Yanga wameendelea na mazoezi yao mjini Morogoro.

Kambi ya Yanga inaandamwa na wachezaji kadhaa walio majeruhi hasa wale wakongwe na tegemeo katika kikosi chake cha kwanza.

Wachezaji ambao ni majeruhi ni pamoja na Thabani Kamusoko, Donald Ngoma na Amissi Tambwe ambao wanatokea Zimbabwe na Burundi.

Kocha George Lwandamina ameendelea kukifua kikosi chake kwa ajili ya mechi ya Jumamosi dhidi ya watani wake.


Mazoezi ya nguvu yanaonekana kupungua na zaidi wachezaji wamekuwa wakichezea mpira zaidi.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic