October 26, 2017




Kikosi cha Simba jana kilishindwa kufanya mazoezi kutokana na mvua kubwa zilizonyesha mjini hapa.

Simba walipanga kufanya mazoezi kwenye uwanja wa jeshi kujiandaa na mechi ya Jumamosi dhidi ya watani wao Yanga, Jumamosi.
Kutokana na kujaa maji yaliyosababishwa na mvua hizo, walishindwa kufanya mazoezi badala yake leo asubuhi wamejifua kwenye Uwanja wa Amaan.
Simba ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara wanajiandaa na mechi hiyo ya Jumamosi dhidi ya watani wake Yanga.

Mechi hiyo imekuwa na presha kubwa kwa kuwa timu hizo zinalingana pointi kila moja ikiwa na 15 lakini Simba inaongoza kwa mabao ya kufunga na kufungwa 'GD'.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic