October 30, 2017


JAFEFR IDDI

Kikosi cha Azam FC kimesema mchezo wao ujao utakuwa mgumu kwa kuwa wanakutana na timu inayotaka kujikwamua kutoka mkiani.

Mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa wikiendi, Azam FC inakutana na Ruvu Shooting ambayo iko mkiani ikiwa na pointi tano tu.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema wataendelea kujiandaa vizuri kwa kuwa wanajua haitakuwa rahisi.

"Wenzetu watakuwa wanapambana kujikoa watoke mkiani. Hivyo kutakuwa na ugumu.," alisema.

"Tayari tumeanza maandalizi ya mechi hiyo na tunaendelea na mazoezi ya ligi kama kawaida na matumaini yetu ni kufanya vizuri."

Azam FC iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 16 sawa na vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba, wanaofuatiwa na Yanga wenye pointi 16 sawa na Mtibwa Sugar wakiwa katika nafasi ya tatu.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic