October 30, 2017



Kikosi cha Ruvu Shooting kimezidi kujichimbia mkiani baada ya kupoteza kwa bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons ya Mbeya.

Wakati Shooting inalala katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Msemaji wa timu hiyo, Masau Bwire amesema wana tatizo la bahati.

“Bahati tu kwa kweli, soka letu lilikuwa kubwa, tulimiliki mpira na kuwapa wakati mgumu sana Prisons.

“Kwa soka ambalo tumeonyesha kila mmoja kaona na ameshangazwa vipi tunapoteza,” alisema.


Ruvu Shooting inaendelea kubaki na pointi 5 ikijishindilia mkiani zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic