November 27, 2017

KIPA wa Mbeya City, Fikirini Bakari, ameibuka na kudai kuwa mshambuliaji  wa Yanga, Obrey Chirwa, hamtishi na hana lolote licha ya  kumfunga hat trick iliyotokana na makosa ya mabeki wake.

Mbeya City ambayo hivi karibuni ilifungwa na Yanga mabao 5-0 huku Chirwa akipiga hat trick, imekuwa haina matokeo mazuri ambapo juzi Jumamosi ilifungwa na Singida United.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Fikirini alisema kuwa licha ya kufungwa mabao hayo lakini mshambuliaji huyo bado ni wa kawaida uwanjani isipokuwa makosa yao ndiyo yamemfanya aonekane bora katika mchezo huo.

“Kikubwa  kilichoniumiza katika mchezo ule ni idadi kubwa ya mabao niliyofungwa, maana sijawahi kufungwa mabao mengi wala hat trick tangu nianze kucheza Ligi Kuu Bara, ile imekuwa ya kwanza.

“Lakini Chirwa aliweza kufunga mabao yale ni kutokana  na makosa ya mabeki wangu na mimi mwenyewe lakini kwangu ni mchezaji wa kawaida, hatishi, isipokuwa imekuwa bahati yake kunifunga vile katika mechi moja ila kwetu tunayafanyia kazi makosa yote,” alisema Bakari.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic