November 13, 2017



Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema beki wao Shomari Kapombe anatakiwa kuanza kucheza la sivyo anaweza kwenda.

Hans Poppe amesema Simba haiwezi kuendelea kumlipa mchezaji ambaye hawatumikii.

“Vipimo vinaonyesha Kapombe amepona, vizuri akaanza kucheza. Hata sisi hatuwezi kuendelea kumlipa mtu ambaye hachezi.

“Sasa tunamuachia yeye, arejee acheze au kama vipi basi aende akajiuguze hadi atakapopona,” alisema Hans Poppe.

Kapombe ameendelea kuwa nje ya uwanja tokea amejiunga na Simba akitokea Azam FC.

Beki huyo wa zamani wa Simba amekuwa akiendelea kujitibia kutokana na majeraha yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic