November 13, 2017



Beki Shomari Kapombe amesema yuko tayari kama Simba watavunja mkataba.

Kapombe amesema hayo akijibu kauli ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, Zacharia Hans Poppe aliyemtaka acheze au aondoke Simba kwa kuwa hawako tayari kuendelea kumlipa bure bila kufanya kazi.

“Mimi ni majeruhi, siwezi kucheza. Kama wanaona wanataka kuvunja mkataba niko tayari.

“Asingekwenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari, angenitafuta mimi ili kujua kinachoendelea,” alisema.

Kapombe amekuwa akiendelea na matibabu tokea ajiunge na Simba akitokea Azam Fc.

Hajapata nafasi ya kuichezea Simba jambo ambalo linaonekana kumuudhi Hans Poppe.


1 COMMENTS:

  1. Ataikumbuka Azam. Saizi angekuwa ashapelekwa South bila masimango. Usimba Na uyanga unawaponza wchezji TZ

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic