November 27, 2017

Baada ya kupata ushindi mfululizo katika uwanja wa nyumbani uongozi wa Singida United umewapa wachezaji wake mapumziko  ya siku saba  huku ikifanyia kazi ripoti ya kocha kwa ajili ya usajili.

 Singida juzi imefanikiwa kuichapa Mbeya City 2-1 katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Namfua na kufikisha jumla ya pointi 20  na ligi imesimama kupisha michuano ya Kombe la Chalenji.

 Akizungumza na Championi Jumatatu, mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo, Festo Sanga, alisema wanajivunia pointi sita walizopata katika uwanja wa nyumbani na wataendelea kupambana licha ya ligi kuwa ngumu.

Kiongozi huyo alisema kuwa si rahisi kupata pointi kwa michezo ya sasa hivi kutokana na  ushindani kuwa mgumu. 

“Tunafurahia matokeo tuliyopata ya ushindi nyumbani, si jambo dogo, zaidi kwa sasa  tumeamua kuwapa wachezaji wetu mapumziko ya siku saba baada ya hapo waturudi kuanza kazi tena na lengo ni kufanya vizuri.

“Kwa upande wa usajili kwa sasa tunaanza kufanyia kazi ripoti ya mwalimu kwa sababu tulikuwa tunasubiri kumalizia mechi hizo kwa sababu tulijua hapa katikati kuna mapumziko na wiki hii mtajua kama tunasajili au tunapunguza,” alisema  Sanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic