November 13, 2017



Msemaji wa Simba, Haji Manara leo ametembelea ubalozi wa Tanzania nchini Oman na kupokelewa na balozi wa Tanzania nchini humo, Abdallah Kilima.

Kilima alimpokea Manara ambaye yuko nchini humo na kuzungumza naye mambo kadhaa kuhusiana na michezo.

“Tumekutana na Balozi Kilima na kumueleza azma ya Simba kufanya vizuri na pia ametupa maneno mazuri ya kutupa moyo.

“Pia tumejadili mambo mbalimbali kuhusiana na michezo mbalimbali na masuala ya kijamii. Hivyo mimi pia nimefarijika sana na nimejifunza mambo kadhaa hapa Oman,” alisema Manara.

Manara alimkabidhi Kilima ngao maalum kama sehemu ya Simba kutoa shukurani kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Oman kutokana na ushirikiano ambao wamekuwa wakiuonyesha kwa klabu hiyo hasa inapotembelea nchini humo.
Ubalozi wa Tanzania nchini Oman umekuwa ukisifika kwa kutoa ushirikiano katika michezo na wanamichezo wanaotembelea nchini humo.

Lakini ni kati ya ofisi za ubalozi ambazo husifiwa kwa ushirikiano kwa Watanzania wanaofika nchini humo kwa shughuli mbalimbali.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic