November 21, 2017



Kamati ua Ufundi na ile ya Usajili ya klabu ya Simba, zinasubiri ripoti ya Kocha Joseph Omog ili kujua mahitaji yake.

Omog bado hahakabidhi ripoti kueleza anataka nini kwa ajili ya dirisha dogo la usajili ambalo tayari liko wazi.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza, Omog atakutana na watu wake wa benchi la ufundi kabla ya kuandaa ripoti.

“Kocha atakutana na watu wake, baada ya hapo atakutana na kamati kwa kutoa ripoti akieleza anataka nini,” kilieleza chanzo.

“Baada ya hapo, basi kamati itaanza kufanya kazi. Ila kwa sasa, bado tunasubiri na tunajua itakuwa baada ya siku chache kwa kuwa tayari kocha amerejea Dar es Salaam kutokea Mbeya.”


Kwa hali ilivyo, inaonekana lazima Simba itahitaji mshambuliaji baada ya Laudit Mavugo kutoka Burundi kuonekana mambo kama yamemshinda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic