November 4, 2017


Pamoja na kwamba Simba itacheza kesho mjini Mbeya, ajabu jezi za wachezaji wake kama Emmanuel Okwi na Jonas Mkude zimekuwa zikinunuliwa kwa wingi mjini Singida.

Gumzo la Singida ni Yanga dhidi ya Singida United leo jioni na jezi za Papy Tshishimbi, Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa ndiyo zinanunuliwa sana.

Lakini mashabiki wengine, wamekuwa wakinunua jezi za Okwi utafikiri Simba inacheza hapa.


Baadhi wamenunua za Mkude ambazo zinaonekana kwisha kwa kuwa wauzaji hawakutegemea itakuwa hivyo.

Hata hivyo wanunuzi wamekuwa wakilalama kukosekana kwa jezi za kutosha za Simba zenye majina mgongoni na wauzaji wamesema wasingeweza kwenda na jezi nyingi za Simba hasa zile zenye majina kwa kuwa wanaamini Yanga kuwa Singida, wengi wangehitaji za Yanga zaidi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic