November 4, 2017





Mauzo ya jezi za wachezaji Papy Tshishimbi yanaonekana kufanya vizuri katika mji wa Singida.

Wengi waliojitokeza kununua jezi za Yanga ambayo itacheza na Singida United leo, wameonekana kununua jezi nyingi zaidi za Tshishimbi.

Tshishimbi ndiye anaongoza kutokana na mashabiki wa hapa Singida kununua jezi kwa wingi.



Lakini mshambuliaji Ibrahim Ajibu, anaonekana kumfuatia Tshishimbi kwa karibu kabisa.

Obrey Chirwa raia wa Zambia, anafunga tatu bora ya manunuzi ya jezi baada ya Tshishimbi na Ajibu.

Jezi za kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donald Ngoma nazo zimekuwa zikinunuliwa kwa wingi licha ya wote wawili kuwa majeruhi.


Yanga itaivaa Singida United leo kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.


TOP 5 YA ZINAZOUZWA SANA SINGIDA:
1. Papy Tshishimbi
2. Ibrahim Ajibu
3. Obrey Chirwa
4. Donald Ngoma
5. Thabani Kamusoko
.

2 COMMENTS:

  1. UPO POA KAKA. MUNGU AKUTANGULIE. TUPO PAMOJA

    ReplyDelete
  2. Huwa nafuatilia sana blogspot yako inanitia moyo sana. mimi mmiliki wa "singidamatukio.blogspot.com"

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic