December 11, 2017




Zikiwa zimebaki siku nne kabla ya usajili wa dirisha dogo haujafungwa, Benchi la Ufundi la Simba limevutiwa kwa kiasi kikubwa na kiwango cha mshambuliaji wa Zanzibar Heroes, Kassim Khamis Seleman anachokionyesha kwenye michuano ya Chalenji huko Kenya.

Mshambuliaji huyo ambaye anaitumikia Klabu ya Tanzania Prisons ya Mbeya, ameweza kuonyesha kiwango kizuri kwenye michuano hiyo baada ya kucheza mechi mbili kati ya tatu na kufunga mabao mawili.

Mechi ya kwanza kufunga bao ilikuwa ni dhidi ya Rwanda wakati Zanzibar Heroes iliposhinda 3-1, huku bao lake la pili aliwafunga Kilimanjaro Stars ambapo pia Zanzibar Heroes ilishinda 2-1.

Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma, amesema amekuwa akiifuatilia kwa kina michuano ya Chalenji na ameona huyo jamaa anawafaa katika kikosi chao.



“Wachezaji wengi ni wazuri lakini huwezi kuwasajili wote lazima uchague kulingana na mahitaji ya kikosi chako. Kwa upande wangu naweza kusema yule straika wa Zanzibar ambaye aliwafunga Rwanda na Tanzania Bara (Kassim Khamis Selemani) ndiye anayetufaa,” alisema Djuma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic