December 24, 2017




Yanga wameendelea kusonga mbele kuwania kulibeba Kombe la Shirikisho baada ya kuitwanga Reha kwa mabao 2-0.

Reha ilionyesha soka safi katika mechi hiyo iliyocheza kwenye UWanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, hadi dakika ya 80 bado ilikuwa 0-0.

Lakini bao la Pius Buswita kabla ya Amissi Tambwe ambaye ametejea baada ya majeruhi, yaliifanya Yanga kumaliza kazi haraka haraka.

Reha walio daraja la pili walijitahidi kuonyesha soka safi na kuzua hofu kwa mashabiki wa Yanga kwa kuwa walikuwa wana kumbukumbu ya kile kilichowatokea watani wao Simba ambao wamevuliwa ubingwa na Green Worriers inayoshiriki Ligi Daraja la Pili pia.


Baada ya kufungwa bao la kwanza, Leha walionekana kupoteza ile hali ya nidhamu kwani dakika chache baadaye wakaruhusu bao jingine na Yanga wakawa wamemaliza kazi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic