January 25, 2018

LIPULI FC

Kikosi cha Lipuli FC kimewasili salama mjini Bukoba kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.

Clement Sanga ambaye ni msemaji wa kikosi cha Lipuli FC, amesema watafanya mazoezi leo na kesho kabla ya mechi hiyo wikiendi.

“Kila kitu kinakwenda vizuri na sasa tutafanya maandalizi ya mwisho kabla ya mechi,” alisema.

“Lengo letu ni kufanya vizuri na tunaendelea kujiandaa kabla ya mechi hiyo. Kikubwa tunawashukuru wote wanaotuunga mkono.”

Sanga alisema mchezaji mmoja ambaye ni majeruhi wamemuacha Iringa lakini wamesafiri na beki wao Mganda George Owino ambaye aliumia mechi iliyopita.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic