January 25, 2018



Mazoezi ya Yanga yanaweza kukuelezea kwamba wamepania kufanya vizuri katika mechi yao dhidi ya Azam FC.

Mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ni nguvu na kazikazi kweli.

Yanga itaivaa Azam FC keshokutwa Jumamosi katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Kiungo Said Makapu ambaye mechi iliyopita alicheza sentahafu, alionyesha si mchezo baada ya kumdhibiti kiungo Emmanuel Martin huku akitaka kupanda mgongoni kwake.

Hata hivyo, Martin naye alikuwa ameonyesha amepania kwelikweli kumpita utafikiri ilikuwa mechi na ushindani mazoezini unaonyesha kuwa wachezaji hao wanataka kushinda mechi hiyo ingawa watalazimika kufanya kazi ya ziada.

Katika mechi iliyopita, Yanga iliigonga Ruvu Shooting kwa bao 1-0 lililofungwa na Pius Buwita.

Hata hivyo, katika mechi hiyo, Yanga haikuonyesha kiwango cha kuridhisha na Ruvu Shooting walipoteza nafasi nyingi za kufunga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic