Kikosi cha Wagosi wa Kaya au Coastal Union kimerejea Ligi Kuu Bara baada ya kuandika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mawenzi.
Katika mechi yake hiyo ya pili iliyopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Coastal Union iliiripua Mawenzi kwa mabao hayo mawil, moja likifungwa na kiungo mkongwe Athumani Iddi ‘Chuji’.
Raizin Ally ndiye aliandika bao moja na Chuji aliyewahi kung’ara na Yanga na Simba akapiga msumari mwingine.
Kwa ushindi huo Coastal Union imefikisha pointi 26 na kujihakikishia kurejea Ligi Kuu Bara.
KUNDI B
P W D L F A GD Pts
1. KMC 14 8 4 2 17 13 4 28
2. Coastal Union 14 7 5 2 18 9 9 26
3. JKT Mlale 14 7 4 3 13 7 6 25
4. Polisi Tanzania 14 6 6 2 18 12 6 24
5. Mbeya Kwanza 14 6 4 4 14 10 4 22
6. Mufindi 14 3 4 7 13 21 -8 13
0 COMMENTS:
Post a Comment