March 8, 2018


Na George Mganga

Mzunguko wa 21 Ligi Kuu Bara unaendelea jioni ya leo kwa viwanja vinne kutimua vumbi jioni ya leo.

Baada ya kuilazimisha sare ya mabao 3-3 Simba katika uwanja wa taifa, Dar es Salaam, Stand United itakuwa mwenyeji dhidi ya Tanzania Prisons, mechi ikichezwa CCM Kambarage, Shinyanga.

Mechi nyingine itazikutanisha Lipuli FC ambayo itawakaribisha Njombe Mji FC katika uwanja wa Sabasaba mjini Iringa.

Nayo klabu ya Majimaji iliyo mwisho mwa msimamo wa ligi, itakuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani kucheza na Ndanda FC.

Aidha Azam FC nao watakuwa katika uwanja wake wa nyumbani, kucheza na Mwadui FC ya Shinyanga. Mpaka sasa Azam wana alama 38 tofauti ya alama 2 na Yanga iliyo na 40, hivyo endapo watashinda leo, watapanda juu na kuishusha Yanga mpaka nafasi ya pili.

Mechi zote zitaanza saa 10:00 jioni isipokuwa ya Azam na Mwadui itakayoanza saa moja jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic