March 19, 2018


Kikosi cha Yanga kimerejea alfajiri ya leo nchini kikitokea Botswana kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kikosi hicho kimewasili majira ya saa 9 usiku kikiwa na msafara wa wachezaji na viongozi wote waliokuwa safarini.

Yanga imeondolewa kwenye mashindano baada ya kukubali kipigo cha jumla ya mabao 2-1 jijini Dar es Salaam dhidi ya Mabingwa wa Ligi Kuu Botswana, Township Rollers.

Katika mchezo uliofanyika huko Bostwana, Yanga ililazimishwa suluhu ya 0-0 na kuipa nafasi Township Rollers kuingia hatua ya makundi.

Baada ya kuwasili nchini leo, mipango ya Yanga hivi sasa ni kujiandaa na Kombe la Shirikisho, Kombe la FA pamoja na Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic