RAKITIC AMKARIBISHA NEYMAR KUREJEA BARCELONA, MILANGO IPO WAZI
Kiungo Mshambuliaji Ivan Rakitic, amesema milango ya Neymar kurejea FC. Barcelona iko wazi.
Neymar aliondoka Barcelona kwenda PSG ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho pauni milioni 198, mwezi Agosti 2017.
Rakitic amesema kuwa, ukiachilia mbali mahusiano yao ya urafiki, anamkaribisha mchezaji kutokana na aina ya uchezaji alionao pia angependa kuona akiwa katika kikosi cha kwanza.
Ni siku kadhaa tu zilizopita kumezuka taarifa za Neymar kutaka kurudi Barcelona, taarifa zinazoelezwa ni kutokufanya vizuri kwa timu yake kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.








0 COMMENTS:
Post a Comment