GUARDIOLA: MANCHESTER HII HAUWEZI KUILINGANISHA NA BARCELONA
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema kuwa si sahihi kuilinganisha klabu hiyo na Barcelona kwa sasa kutokana utofauti wa mafanikio uliopo baina ya vilabu hivyo.
Guardiola ambaye aliwahi kuiona Barcelona na kuipatia mafanikio makubwa, ameeleza kuwa man City mpaka sasa ina taji moja pekee tofauti na timu yake ya zamani.
Kocha amesema kuwa ni mapema sana kufanya mlinganisho huo kutokana na Barcelona imekuwa ikichukua mataji kila nyakati na imetawala soka kwa miaka 10 mpaka 15 ikiwa na Makocha tofauti.
Ukiachilia wachezaji, Guardiola pia ameeleza wachezaji tofauti-tofauti wameisaidia Barcelona kuwa na mafanikio makubwa kwa kipindi chote hicho.
"Kila msimu wamekuwa wakishinda mataji, tofauti na sisi tulio na taji moja pekee 'Carabao Cup', kujilinganisha na timu kama Barcelona inabidi uchukue safari ndefu kuwafikia", alisema Guardiola.
Manchester City inaingia kucheza mchezo wa marudiano usiku wa leo kwenye hatua ya 16 bora dhidi ya FC. Basel, ambao katika mchezo wa kwanza walishinda jumla ya mabao 4-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment