March 7, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha Simba kinashuka dimbani jioni ya leo katika uwanja wa taifa kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry kutoka Misri.

Al Masry inaenda kucheza na Simba ikiwa nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi nchini Misri huku ikiwa na mechi mbili mkononi.

Wakati huohuo Simba wanaingia uwanjani wakiwa na rekodi nzuri ya kutopoteza mechi yoyote katika ligi, na wakiwa kileleni mwa ligi kwa alama 46.

Simba watapaswa kupata matokeo leo ili wajiwekee nafasi ya kusonga mbele katika mchezo wa marudiano utakaopigwa baada ya siku 10 ama 11 zijazo.

Kufuatiwa kuanza vibaya kwa Yanga jana katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba wanapaswa kutumia mapungufu ambayo Yanga walionesha mechi ya jana kama funzo ili wapate matokeo leo.

Ni dhahiri shahiri fitina na figisu za soka la Waarabu zinajulikana huzifanya wakiwa kwao, ili kuepuka hayo leo, wanapaswa kutumia faida ya uwanja wa nyumbani leo.

Uwepo wa John Bocco na Emmanuel Okwi endapo watacheza unaweza kuwa chachu ya morali uwanjani, kutokana na uzoefu walionao katika mashindano ya kimataifa.

Kikubwa wanacholazimika kukifanya ni kupambana ili wapate mabao mengi ili kujiwekea faida kwenye mchezo wa marudiano.

Mechi hii itaanza majira ya saa 12 jioni na itakuwa mbashara kupitia kituo cha Azam TV. 

Nichukue nafasi hii kuitakia kheri Simba SC.




5 COMMENTS:

  1. Hata Yanga ina nafasi ikijipanga vyema, KILA LA HERI SIMBA

    ReplyDelete
  2. Kila kheri Simba hata Shari ikibidi kutumika ili kujijengea heshima sawa tu. Nawafahamu Wamisri vizuri sana. Simba waache kabisa kuwa na mawazo labda wanacheza na Maimamu au Masheikh,hapana utaona hata wao wenyewe wanajiita Mafirauni. Wamekuja Tanzania wamekuja vitani hawana cha msalie mtume. Wanaweza wakatumia muda mwingi kujilinda na kushambulia kwa kushutkiza watakapoona kuna nafasi hasa kupitia wachezaji wao wa pembeni. Na wazuri sana wa mipira ya kona na mafundi sana katika set pieces. Wanaweza kutumia mbinu za kupoteza muda mapema tu ili kujiandaa kuwasubiri Simba Misri. Wachezaji wa Simba wasipo jituma kuendana na kasi yao kunaweza kuwagharimu. Lakini kwa kuwa simba ina nguvu zaidi ya mashabiki hapana shaka matokeo yatakuwa mazuri kwa upande wetu InshaAllah.

    ReplyDelete
  3. Beki ya Simba wawe wepesi sana kuondoa mipira kwenye goli lao. Wamisri ni wajanja mon kosa moja goli. Simba wasibweteke wajitume na kupeleka mipira mbele.

    ReplyDelete
  4. Haya mnyama tunataka kuusikia mngurumo wako wa kulitikisha bara la Africa. Mungu na jamhuri pamoja nanyi

    ReplyDelete
  5. wasiwasi wangu ni kwa golikipa najua wamisri wameshajua Manula za mbali hafuati pia beki ya simba ni ngumu,hivyo naomba Manula awe macho pia beki zijipange sana kuzuia magoli ya mbali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic