March 7, 2018



Na George Mganga

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, amesema kuwa kuwa Yanga walipoteza mchezo wa jana dhidi ya Township Rollers sababu walikuwa bora.

Akihojiwa na Mwandishi wa EFM, Mussa Mwakisu, Mwakyembe alieleza kuwa Yanga walikuwa hawana mshikamano mzuri uwanjani, kitendo ambacho kilisababisha kupoteza mipira mara kwa mara, huku akitumia neno "mipira iliwaponyoka'.

Yanga imeshindwa ktumia Uwanja wake wa nyumbani katika mchezo huo siku ya jana kwa kufungwa mabao 2-1 na kujiwekea mazingira magumu kwenye mechi ya marudiano.

Ukiachilia hilo, Mwakyembe pia aliulizwa kuhusiana na uwekezaji katika vilabu vya Tanzania, ili vifanye vema katika mashindano ya kimataifa, alisema Yanga wanapaswa kufanya hivyo kwani tayari Simba wameshafanikisha.

Mwakyembe ameshauri ni vema tu wakafuata taratibu za uwekezeaji lakini hakuna atakayezidi asilima zaidi ya asilimia ambazo zimewekwa na serikali.

Chanzo cha Habari - EFM

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic