HAJI MANARA SEMA YANGA WAMEJITAKIA WENYEWE KUFUNGWA, ADAI WALIJIKITA KUIZUNGUMZIA SIMBA
Na George Mganga
Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amezungumzia matokeo ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliowakutanisha Yanga dhidi ya Township Rollers ya Bostwana Jumanne ya leo.
Akizungumza na kipindi cha E Sports kupitia radio EFM ya Dar es Salaam, Haji amesema Yanga amesema kuwa wamepoteza kizembe kutokana na kutumia muda mwingi kuongelea mechi ya Simba tofauti na kujadili namna ipi watapambana na Township Rollers.
Kauli hiyo imekuja mara baada ya Yanga kupoteza mchezo wa leo kwa mabao 2-1 na kujitengenezea mazingira magumu kusonga kwenye mcheo wa marudiano ambapo Yanga italazimika kushinda mabao matatu kwa 0.
Haji Manara ameshauri pindi panatokokea mechi za kimataifa kama hizi, ni vema vilabu vikaungana kuwa taifa moja na kupeana hamasa badala ya kuleta matabaka.
Baada ya mchezo huu, Simba nao kesho watakuwa Uwanja wa Taifa kucheza dhidi ya waarabu, Al Masry SC ya Egypt.
kwani bila ya kuizungumzia Yanga utaonekana sio Msemaji wa Simba
ReplyDelete