March 6, 2018


Na George Mganga

Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers ya Botswana, umemalizika katika Uwanja wa Taifa kwa wenyeji kupoteza kwa jumla ya mabao 2-1.

Katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, Township Rollers ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kwanza mapema kabisa kwenye dakika ya 11 kupitia kwa Lemponye.

Baada ya bao hilo la kuongoza kwa Rollers, Yangan waliendelea kupambana ambapo katika dakika ya 30, mshambuliaji Obrey Chirwa aliweza kufunga bao la kusawazisha, kufuatia kazi nzuri ya Papy Tshishimbi aliyetoa pasi kwake.

Mpaka mwamuzi anapuliza filimbi ya kumaliza kipindi cha kwanza, matokeo yalikuwa ni 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kushambuliana kwa zamu, ambapo nyavu hazikuweza kutikisika mapema, ambapo ilichukua muda mpaka zikasalia dakika 7 zikisalia kuelekea mwishoni mwa mchezo, Sikela akafunga bao la pili kwa Rollers katika dakika ya 83.

Mpaka dakika 80 zinamalizika, Yanga walikuwa nyuma kwa mabao 2-1.

Matokeo hayo yanaipa wakati mgumu Yanga kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa huko Gaborone Botswana, ambapo watabidi washinde mabao zaidi ya mabao mawili kwa sufuri ili waweze kusonga mbele.

4 COMMENTS:

  1. Yanga wanayo nafasi bado ya kushinda goli 3 - 0 kwenye mechi ya marudiano endapo watasahihisha makosa madogomadogo na kufanya mazoezi ya kutosha.

    ReplyDelete
  2. Timu yeneywe ya yanga iko wapi ya kwenda kuwafunga wale waswana kwao goli tatu3? Yanga haikuwa na maandalizi yeyote ya maana ya kupambana katika ligi ya mabingwa tangu mwanzo wa msimu. Wale washelisheli wazembe tu lakini walikuwa waiondoshe yanga mapema tu. Yanga kazi kun'gan'gania ubingwa wa ligi hata kwa mizengwe lakini siku zote wamekuwa na uwakilishi wa hovyo kimataifa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tufanye simba ndio mabingwa basi, unaleta unazi badala ya kujadili fact iliyotolewa hapo juu. Makosa madogo madogo ndio yamesababisha yanga kufungwa pia kumbuka yanga ina majeruhi karibu sita tena ya key players unategemea kuwa bado yanga watakuwa on fire kimataifa? Juzi tu hapa kuna timu ilikuwa na majeruhi wawili lakini ulimi ulikuwa nje nusura wapoteze je ingekuwa wao wapewe viatu vya yanga si ingekuwa katika mstari wa kushuka daraja...

      Delete
    2. Rekodi zote tangu kuumbwa kwa dunia au vita kuu ya pili ya dunia inaonyesha kwamba yanga ni timu ya kuchukua ubingwa wa TFF tu yaani kombe la Tanzania kwa mizengwe ya akina MALINZI na sio timu ya kushiriki kimataifa ambako hakuna mizengwe na ndio maana iliponea chupuchupu kwa wale washelisheli ambao bado wanajifunza soka. Mara zote yanga uanza mechi za kimataifa na either Comoro au mataifa mengine yanayojifunza soka na uwa inashinda japo kwa taabu lakini ikifika raundi ya pili uwa ndio mwisho wao. Nahauri wacha yanga iwe inachukua kombe la TFF miaka yote. Simba itabaki kuwa ya kimataifa kwa maana mpk dakika hii niandikapo ujumbe huu ndio timu inaongoza kombe la shirikisho Afrika nzima! Angalia rekodi yake ya magoli ya kufunga na ya kufungwa na ifananishe na timu ntingine yoyote unayoijua kaika bara zima la Afrika! Simba wacha wae wa kimataifa na yanga wawe mabingwa wa TFF kila mwaka

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic