March 7, 2018



Kocha Pierre Lechantre, ameingiwa na hofu kidogo juu ya muda wa mechi yao ya leo dhidi ya Waarabu wa Al Masry kwa kile alichosema wachezaji wake hawana uzoefu na kucheza muda huo lakini watapambana.

Simba na Al Masry watapambana leo Jumatano kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya kwanza utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar kuanzia saa 12 jioni.

Ili kuizoea hali hiyo ya kucheza jioni sana, juzi Jumatatu Simba ilianza mazoezi yake saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Boko uliopo jijini Dar es Salaam, lakini ghafla Lechantre akakatisha mazoezi hayo kwa kuhofia wachezaji wake kuumizana kutokana na giza.

Hata hivyo Uwanja wa Boko una taa ambazo mara nyingi zimekuwa zikitumika kwa mazoezi ya usiku, lakini zilionekana kuwa hafifu jambo lililomtisha kocha huyo.

Lechantre alisema: “Nimelazimika kukatisha mazoezi kwani taa za hapa hazina mwanga mzuri, wachezaji wangu wanaweza kuumizana. Mpaka sasa sijui ni nani ambaye amepanga mechi yetu hiyo tucheze muda huo wa kuanzia saa 12.”

“Wakati mwingine inaweza kuwa ni bora kwenu kucheza usiku wakati mwingine ni mbaya. Kwa sasa hatujali sana kuhusiana na huo muda kwa sababu ishapangwa, ninachokiangalia ni kuiandaa timu kuwa bora,”alisema kocha huyo juzi usiku.

“Kitu kizuri ni kwamba katika safu yangu ya ushambuliaji nina Bocco na Okwi ambao watasaidia kwenye mashambulizi nafikiri inatosha niwashukuru kwa kuja.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic