March 7, 2018





Joseph Omog aliyewahi  kuwa Kocha Mkuu wa Simba, ana imani kubwa inaweza kushinda leo dhidi ya Waarabu wa Misri.

Simba inaivaa Al Masry ya Misri katika mechi ya Kombe la Shirikisho itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kutoka kwao Omog alisema; “Nawatakia kila la Kheri Simba katika mchezo wao huo na wanaweza kushinda wakijipanga vyema, naijua  Al Masry ni timu nzuri.”

Omog aliondoka Simba baada ya kuiwezesha kuwa bingwa wa Kombe la Shirikisho na kuirejesha kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kuikosa kwa miaka mitano.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic