LIGI KUU BARA KUENDELEA TENA, MECHI HIZI ZINAPIGWA JIONI YA LEO
Na George Mganga
Ligi Kuu Bara inataraji kutimua vumbi tena Jumatano ya leo kwa mechi kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti.
Jijini Mbeya, Mbeya City leo watakuwa wenyeji dhidi ya Mbao FC iliyosafiri tokea jijini Mwanza ambapo mechi itapigwa kwenye Uwanja wa Sokoine. Mechi itaanza saa 10:00.
Aidha, Singida United nayo itakuwa katika uwanja wake wa nyumbani ikiikaribisha Ruvu Shooting, mechi ambayo pia itaanza saa 10 kamili jioni.
Mechi hizo ambazo ni za mzunguko wa 21, zitaoneshwa moja kwa moja na kituo cha Azam TV.
0 COMMENTS:
Post a Comment